Mwaisambe alipata taarifa kwamba katika jimbo lao la Matusitusi kulikuwako na mganga mashuhuri. Mganga huyo aliwatibu watu kwa dawa za kienyeji alizokuwa nazo daima. Basi baada ya kusikia habari kumhusu mganga huyo, Mwaisambe aliamua kwenda kumtembelea. Ndugu Mwaisambe anaonekana kuishi maisha ya kubahatisha. Ni mfano wa vijana wanaoonekana kukosa ruwaza, wanabebwa hobelahobela na upepo wa nakama na kuwaangamiza. Mwaisambe yu safarini kumtafuta mganga mashuhuri asiyemjua asili wala fasili yake. Anapanda milima na kuivuka miamba hadi katika eneo la Kivunja Kimya. Atafaulu kumpata mganga wake? Jisomee upate kujua...