image description
# 841131
USD 20.00 (Book in Stock, will be dispatched ASAP)
- +

Chachu za Waja

Author :  Muhindo Augustine ‘Bin' Mali

Product Details

Country
Kenya
Publisher
Nsemia Inc. Publishers, Kenya
ISBN 9789966082794
Format PaperBack
Language Swahili
Year of Publication 2022
Bib. Info x, 166p.
Product Weight 250 gms.
Shipping Charges(USD)

Product Description

Udhalimu wa wanawake na wanaume ni suala la kawaida. Kazi hii inadhihirisha uhalisia wa maisha katika familia nyingi za kisasa ambapo kuna ufeministi ambapo hata mwanamke anahisi kuwa nguzo ya familia. Maisha hayo ni sawa na yale watu waliyokuwa wakiishi katika nchi dhahania ya Sokoya, iliyokuwa na makabila mawili yaani Wakomoro na Warambi. Riwaya yenyewe, inadhihirisha dhahiri shahiri jinsi wanaume wanavyodhulumiwa na wake zao. Bw. Mkata ni mfano bora anayedhalilishwa na mkewe Zekelina, mwanamke mashuhuri na maridadi katika mavazi yake kwa sababu ya hali yake ya uchechefu wa pesa. Latifu pia anadharauliwa na mchumba wake Firinda anayetambua kuwa hajatahiriwa kwa mujibu wa utamaduni wa Rambi. “....ujue kwamba sikutaki tena nyumbani kwangu, muda wako uliisha zamani. Wewe kwa kweli si wa hadhi yangu.” Alisema Firinda akimfukuza Latifu. Latifu alilia akadondokwa na machozi mengi yaliyomlowa mwili mzima, na kutiririka hadi yakaunda kijito cha maji. “Kweli mapenzi uchizi! Kwa nini umekuja katika maisha yangu ili uniumize? Kwa nini umeruhusu moyo wangu akupende halafu uje kuniacha njiani? Ina maana wakati ulinishawishi nikupende hukuyajua haya...” Kinyume na matarajio, mahusiano yanazuka wakati ambapo wanawake wanawapenda wanaume na kuvuka mipaka na kutangaza hisia zao. Peremina anamchumbia Isma naye Firinda anamsalitikia Latifu na mahusiano hayo mawili yanaishia kwenye machozi.

Product added to Cart
Copied