Country | |
Publisher | |
ISBN | 9789914962017 |
Format | PaperBack |
Language | Swahili |
Year of Publication | 2022 |
Bib. Info | v, 96p. |
Categories | Literature |
Product Weight | 150 gms. |
Shipping Charges(USD) |
Kwikwi za vilio vya bi harusi zinasikika kwa mbali. Kalazimishwa kuwa mke wa mtu, ndoto yake imevunjwa na kusagwasagwa bila ya huruma. Kavalishwa gauni la kiyombo, kichwani katundikwa taji la leso lililopachikwa viwangwa vinavyongaa. Machozi yanamtoka machoni na kuuharibu wanja aliopakwa. Naam machozi. Si machozi ya furaha bali ya karaha. Binti wa miaka kumi na mitatu hatimaye anaenda kufunga ndoa na mzee wa miaka tisini. Je huu ni mwisho wa ndoto yake Bi harusi aliyoiwekeza toka angali kinda? Ama ndio mwanzo wa shida zake kuisha? Mwanzo wa Mwisho ni riwaya iliyojikita nchini Fokota. Wanawake wa jamii hii wametengwa na kudharaulika. Wao hawana kauli mbele ya wanaume. Mateso, binti aliyekulia kwenye utandabui wa unyanyapaa alijikusuru kuingoa mizizi hiyo. Je atakumbana na yepi njiani? Na je atafaulu?